Loading...
×

Loans Calculator

Calculate interest base on

Expert Loan Tips

Before you apply for a personal loan, consider other forms of credit. You might find a credit card is cheaper and a card with a 0 per cent introductory offer on purchases will enable you to spread the cost of big purchase interest-free.

*The rates above are indicative, visit a branch near you for more details.
Benki ya Equity Tanzania inazindua suluhisho jipya ya benki kimtandao

Dar es Salaam, 19th feb, 2018 – Benki ya Equity imezindua huduma za benki kwa njia ya kimtandao, huduma hizi zilizopewa jina “Eazzy Banking” zitawawezesha wateja wa benki kupata huduma za kibenki kwa njia ya mtandao popote walipo, muda wowote watakapo hitaji, kupitia simu zao za mkononi, vifaa vingine vya mawasiliano kama tablets au Ipads na compyuta za mezani au laptop.

Huduma hizi mpya za kibenki zitatoa suluhisho kwa wateja kufanya miamala kirahisi iwe usiku au mchana, kupata huduma za kibenki wakiwa nyumbani au ofisini, kuokoa muda na gharama. Wateja watanufaika na urahisi, uwezo na uhuru wa kuchagua jinsi gani ya kufanya miamala yao ya kibenki.

Huduma za eazzy Banking zitaambatana na EazzyBanking App, app ya kimataifa ya maswala ya kifedha inayounganisha huduma za laini za simu na kuwawezesha wateja kutuma fedha na pia kufanya malipo kupitia simu zao popote walipo, wakati wowote. App hii inapakuliwa/downloaded na baadae kwa vifaa vya IOS; App ya EazzyBanking ni rahisi kuianzisha(activate) na hutoa huduma za kipekee kama kutuma fedha kwenda akaunti za benki au mitandao ya simu, kuomba na kulipia mikopo, kulipia bili na vingine vingi.

Kwa wale walio na simu za kawaida, kuna suluhisho kwao, linajulikana kama Eazzy24/7. Huduma hii iliyoboreshwa inawawezesha watumiaji kupata huduma zile zile kama za EazzyBanking app kwa kupiga *150*07# kupitia simu zao.

Huduma hii pi huambatana na sehemu mtandaoni kufanya manunuzi za reja reja ambapo wateja wanaweza kuendesha akaunti zao hii inajulikana kama EazzyNet; huduma ya malipo mbalimbali inayoitwa EazzyPay, huduma hii inakuwezesha kufanya malipo ya bili kama ya Ving’amuzi mfano StarTimes, DStv, Zuku, Tanesco(LUKU na Dawasco. Pia unaweza kununua na kulipia bidhaa na huduma kupitia kwa wauzaji waliosajiliwa kama SuperMarket na Hoteli pale unapoona bango au stika ya “EazzyPay inakubalika hapa”; Huduma ya Mkopo kwa njia ya simu inayoitwa EazzyLoan; pamoja na ufumbuzi na usimamizi wa fedha kwa SMEs na Wateja wakubwa na makampuni makubwa au wizara inayoitwa EazzyBiz.

Kwa kuongezea, kuna EazzyKikundi, suluhisho kwa kuwasaidia SACCOs, VIKOBA, vikundi vya kiuchumi na uwekezaji na utunzaji kumbukumbu za biashara.

Akiongea siku ya uzinduzi, Mr Joseph Iha, Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Equity Tanzania, alisema huduma ya Eazzy Banking itawawezesha wateja kupata huduma za kibenki kiurahisi, kiusalama na bila stress.

Mkurugezi Mtendaji aliongeza, uzinduzi wa huduma hii ya kibunifu unaongozwa na huduma Mama ya EazzyBanking App ambayo itaimarisha mbinu ya mkakati wa benki katika kuwahudumia wateja  kimtandao  kutokana na mabadiliko ya mahitaji yao.

“Hii imejulikana kutokana na mienendo ya kibenki ya wateja, ambayo imeonesha kukua kwa huduma binafsi zinazowawezesha kubenki popote, muda wowote. Anachotakiwa kufanya mteja ni kupakua tu EazzyBanking App na upate urahisi wa kubenki. Aliongeza kuwa: “ kupitia EazzyBanking App, mteja pia anaweza kuomba mkopo unaojulikana kama EazzyLoan na baada ya sekunde kadhaa watapata mkopo huo kwenye simu zao. EazzyBanking App ni suluhisho la kuwasaidia wateja kuishi bila stress bure ambapo miamala itafanyika haraka papo hapo”.

Uzinduzi wa huduma za EazzyBanking unakuja kipindi ambapo benki ya Tanzania  imeonyesha faida za fedha za mtandao kataka kukuza huduma za fedha na ukuaji chanya wa maswala ya kiuchumi.

Kwa kuongezea, kwa maeneo ya kanda, uzinduzi huu umekuja kwa haraka kama ilivyokuwa kwa benki ya Equity Uganda, Rwanda na Kenya ambapo Benki inatadhamia kuongoza katika sekta ya kimtandao kwa maswala ya kibenki ndani ya Afrka Mashariki na kati.

Kwa mujibu wa ripoti ya kila mwaka ya Benki ya Tanzania 2016/17, licha ya ukuaji wa taratibu wa fedha kwa shughuli za kiuchumi, kulikuwa na ongezeko la thamani ya fedha katika mzunguko wa fedha ambao ulitokana na matumizi ya huduma za fedha za mtandao kwa Watanzania wakati wa ukaguzi.

Kwa mujibu wa mdhibiti, idadi ya akaunti za kazi katika huduma za fedha za mtandao zilifikia milioni 17.5, na mawakala zaidi ya 300,000.

Mwisho/…

 

Kwa maelezo Zaidi tafadhali wasiliana na

 

Betty E. Kwoko

Equity Bank Tanzania Ltd

Office 0768 985500

E: betty.kwoko@equitybank.co.tz

E: corporatecommunications@equitybank.co.ke

Myoma Kapya

J Walter Thompson Tanzania

T. 0677042633

E. Myoma.Kapya@jwt.co.tz  

 

Kuhusu Benki ya Equity Tanzania

Equity Bank Limited – Tanzania, ni benki ya Biashara iliyoidhinishwa na kusimamiwa na Benki ya Tanzania

Benki ilianzisha shughuli zake mwaka 2012. Kwa sasa ina matawi 15 yaliyotawanywa Dar es Salaam, Arusha, Moshi, Mwanza, Dodoma, Zanzibar, Mbeya na Morogoro mikoa yenye mipango ya upanuzi. Mtandao wa matawi unasaidiwa na mawakala zaidi ya 1,300 na wafanyabiashara pamoja ATM 15. Banking Equity Bank ina shughuli zake nchini Uganda, Sudan Kusini, Rwanda, DRC na Kenya. Maono ya Benki ya Equity ni kuimarisha ufanisi wa kiuchumi kwa jamii ya watu wa Afrika huku lengo lake likiwa kubadilisha maisha ya watu kijamii na kiuchumi kwa kuwapa huduma za kisasa za kifedha ambazo zitaongeza fursa kwao.

 

Kwa habari zaidi kuhusu Benki ya Equity, tafadhali tembelea tz.equitybankgroup.com

Be the first to comment of this article.
0

You need to login to comment. Login in with either:

Quick way to access your cash

Money Transfer Across the World