Loading...
×

Loans Calculator

Calculate interest base on

Expert Loan Tips

Before you apply for a personal loan, consider other forms of credit. You might find a credit card is cheaper and a card with a 0 per cent introductory offer on purchases will enable you to spread the cost of big purchase interest-free.

*The rates above are indicative, visit a branch near you for more details.
Equity Bank Tanzania limited imeingia ubia na Klabu ya Simba

Dar es Salaam, 14th December 2019… Equity Bank Tanzania limited imeingia ubia na Klabu ya Simba katika kutoa kadi zenye chapa zao kwapamoja ambazo zinafaida kwa mashirika yote mawili lakini walengwa wakuu ni watakao kuwa wamiliki wa kadi hizo ambao ni wateja/mashabiki na wadau wa mashirika haya mawili kwa umoja wao.

Klabu ya Simba inashauku kubwa kuwapa shabiki/ wadau wake kadi zitakazo warahisishia huduma za malipo mbalimbali, kuweka akiba, kutoa na kuweka hela Benki. Equity Bank dira na dhimaa yake itakuwa Dhahiri kubadilisha maisha ya watanzania kijamii na kiuchumi pia kuongeza idadi ya wanaopata huduma za kibenki nchini.

Akaunti inayompatia shabiki wa Simba kadi ya shabiki (Simba Debit card) pia ina faida zifuatazo;
•    haina kiwango cha chini cha kulinda akaunti
•    haina makato ya mwisho wa mwezi
•    haina makato ya kuweka hela hali kadhalika
•    haina makato ya kuweka hundi na pia kupata huduma za kifedha kupitia simu za mkononi.
•    Kadi ya shabiki wa Simba pia ina faida ya kipekee kuwa imeunganishwa na mfumo wa VISA utakaomuwezesha mmiliki wa kadi hii kupata huduma za kifedha popote penye nembo ya VISA ndani na nje ya nchi. Kama benki, tunajivunia ubia wetu na klabu ya Simba.

Kupata kadi hii mtu anastaili kufata utaratibu mzima wa kufungua akaunti ya Benki kwa kutumia kitambulisho cha taifa (NIDA) au namba ya NIDA ama Kitambulisho cha kupiga kura.

Mteja ataitajika kuchangia pesa taslimu zakitanzania Tzs 22,000 kama kianzio cha kupata kadi ya Simba, ambapo Tzs 10,000/= ni malipo ya kadi na Tzs 12,000 ni ada ya shabiki wa simba kwa mwaka mzima.

Kadi zinazotolewa sasa ni kadi za mashabiki, na siku za usoni kadi za wanachama/wadau zitafuata. Utoaji wa kadi unafanyika kwenye matawi yote ya Equity Bank Tanzania, na sehemu ambapo hakuna tawi la Equity Bank Tanzania mpango mkakati unafanyika na ratiba ya kuzungukia sehemu hizo utatangazwa rasmi.

Tunapenda kukukaribisha kwenye toleo letu jipya la Simba Debit card. Kadi hii inakuja na faida za nyongeza kwa mashabiki na wanachama wa Klabu ya Simba.

Ukiwa na kadi ya Simba Debit Card utafurahia huduma zifuatazo;
•    Kitambulisho cha mwanachama
•    Kuweza kufanya miamala ya kutoa na kuweka fedha, manunuzi na malipo ya mtandaoni
•    Kupata punguzo utakapo fanya manunuzi katika maduka pendwa
•    Manunuzi ya Ticket za Mechi
•    Manunuzi ya bidhaa za Simba
•    Makato ya papo kwa hapo ya malipo ya mwanachama
•    Kuingia katika uwanja wa mpira wakati wa Mechi
•    Kubenki kielektroniki


Equity Bank Tanzania limited ilianza shughuli zake mwaka 2012 baada ya kuchagua na kuwaelimisha vijana wa kitanzania wapatao 80 nje ya nchi kwa takribani mwaka mmoja. Mpaka sasa, tunayo matawi 15 na mawakala wanaozidi 2,800, huduma ya simu (Eazzy Banking) ambayo inamuwezesha mteja kuendelea na miamala yake popote alipo kwa kutumia simu yake ya mkononi.

Dira yetu ni kuwa mstari wa mbele katika kuboresha maisha ya kila mwafrika kiuchumi na kijamii. Ni kwa kuzingatia dira hii ambapo tumekuwa tukibuni huduma zinazoendana na soko letu, hali ya maisha ya watu wetu lakini pia kasi ya teknologia duniani na hata wakati mwingine kufikia kuleta huduma ambazo wengi waliomo katika biashara ya utoaji wa huduma za kifedha kuziona kuwa hatarishi.

Equity Bank Tanzania inakaribisha maoni na ushauri ili kuzidi kuboresha huduma zetu kwako. Tutaendelea kujitolea katika kuhakikisha unapata huduma bora.

Asante kwa kuichagua Equity Bank.
*vigezo na masharti kuzingatiwa

Be the first to comment of this article.
0

You need to login to comment. Login in with either:

Quick way to access your cash

Money Transfer Across the World